Watu waliokimbia makaazi yao kutokana na vita nchini Sudan Kusini, wakisubiri maboti kuvuka mto Nile, katika mji wa Bor.
Mapigano yanaendelea nchini Sudan Kusini licha ya pande mbili zinazohusishwa na mgogoro wa nchi hiyo kujiandaa kwa mazungumzo ya amani nchini Ethiopia.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini ameiambia BBC kuwa mapigano yanaendelea katika mji wa Bor na baadhi ya sehemu za jimbo la Unity.